Wana JF hii nimeipata kupitia Blog ya Abdallah Mrisho .
Source:Gazeti la Amani
Kiasi cha shilingi bilioni 1.4 kinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa nyumba ya kifahari (hekalu) ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (F.G.B.F), Zacharia Kakobe, kufuatia michango iliyotolewa na waumini wake, Amani limeelezwa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, uchangishaji huo kwa ajili ya zoezi hilo umekuja kufuatia ombi la kiongozi huyo kutaka waumini wamnunulie gari kutokana na lile alilokuwa akitumia kuchakaa.
Ilielezwa kuwa, kufuatia ombi la Kakobe, waumini hao wakishirikiana na wafanyabiashara mbalimbali waliowahi kufanyiwa miujiza ya kiroho na kiongozi huyo waliamua kuchanga fedha kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo.
Aidha chanzo hicho kimezidi kufafanua kuwa, waumini hao licha ya ombi la kiongozi wao kutaka anunuliwe gari pia waliona ni vema kumjengea nyumba ambayo itaendana na hadhi aliyonayo.
"Licha ya yeye kuomba kusaidiwa kununuliwa gari, waumini pamoja na wafanyabiashara mbalimbali wa Dar es Salaam na mikoani waliahidi kuchangia kwa ajili ya kumjengea nyumba ya heshima kufuatia ile ya Kijitonyama, Dar es Salaam, kutokuwa na hadhi," kilidai chanzo hicho.
Chanzo hicho cha habari kilizidi kueleza kuwa, waumini hao wamedhamiria pia kuwanunuliwa magari watoto wa kiongozi huyo kwa ajili ya kutembelea.
Habari zinadai kuwa, katika kufanikisha zoezi hilo, maaskofu wa mikoa mbalimbali nchini walikutana mkoani Dodoma mwanzoni mwa wiki iliyopita kufanya tathmini ya michango hiyo ambapo ilibainika kuwa kiasi cha shilingi bilioni 1.4 kilikuwa kimeshakusanywa.
Wakizungumza na Amani kwa masharti ya hifadhi ya majina yao, baadhi ya maskofu hao wamethibitisha kufanyika kwa michango hiyo na kueleza kuwa, lengo hasa ni kuhakikisha kiongozi wao anakuwa na maisha mazuri.
"Tuliguswa sana pale makazi ya kiongozi wetu yalipooneshwa kwenye televisheni moja na kuona kwamba anaishi kwenye nyumba isiyorandana na heshima aliyonayo katika jamii.
"Ukichukulia kwamba, viongozi wanaweza kumtembelea nyumbani kwake ikawa aibu, ndio maana tumeamua kuendesha zoezi hilo," alisema mmoja wa maaskofu hao.
Amani lilifanya jitihada za kumtafuta Askofu Kakobe ili kuzungumzia zoezi hilo lakini hakuweza kupatikana mara moja. Hata hivyo, wakati kiongozi huyo akichangiwa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo uchunguzi umebaini kuwa, baadhi yao hawana hali nzuri sana ya kimaisha.
Licha ya waumini hao kuwa katika hali hiyo, mapenzi ya dhati kwa kiongozi wao ndiyo yaliyowasukuma kutoa michango yao bila kulazimshwa. Kanisa F.G.B.F ni moja kati ya makanisa makubwa ya kiroho nchini Tanzania.
Kweli waungwana Iman itakuwepo kweli? maana "hata kama hatujui Kusoma Hata kuangalia Picha basi"
Source - Abdallah Mrisho
Friday, October 5, 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment