Saturday, October 6, 2007

Mlevi

Walevi walikuwa wanasikiliza taarifa ya habari kuhusu mambo ua uzazi nchini China; Msomaji wa habari alikuwa anaelezea kama ifuatavyo: Uko Uchina kila dakika moja kunazaliwa mtoto...!

Mlevi: he!he!he! ndio ujuwe hao watu wameendelea na ndo kuna wanaume na wanawake wa shoka huko, sio wanawake wetu hapa wanabeba mimba kila miezi tisa ndo mana tupo nyuma...!
__________________

Wakazi wa dunia ni mbwa wabwekao
na
wanyama wa mwitu wangurumi-a-nao.
Wenye nguvu huwala walio dhaifu,
Wakubwa huwagandamiza wadogo.
Ni kama mifugo, wengine wamefungwa
na
wengine hawakufungwa.

0 comments: