Na Joseph Mwendapole, Ukerewe
Wakazi wa Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, wametoa mpya pale walipomweleza Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa, kuwa ulaji wa samaki pamoja na kunywa supu yake ndicho chanzo cha kuenea kwa Ukimwi kwa kasi visiwani hapo.
Wananchi hao wanaeleza kuwa unywaji wa supu ya samaki zinazopatikana kwa wingi wilayani hapo unachochea watu kuhamasika na kupenda ngono kwa kiwango kikubwa.
Hayo yalijitokeza wakati wa mkutano wa hadhara katika Shule ya Sekondari ya Pius Msekwa, mara baada ya Bw. Lowassa kuhoji sababu za kuenea kwa kasi kwa ugonjwa huo.
Alipouliza swali hilo, watu wengi waliohudhuria mkutano huo walilipuka kwa sauti kubwa kuwa ``ni supu ya samakiii.``
Bw. Lowassa aliwaonya kuwa maambukizi katika visiwa vya Ukerewe ni makubwa yamefikia asilimia 20 tofauti na wastani wa taifa ambao ni asilimia saba.
``Nilipokwenda Makete ambako nako Ukimwi umepamba moto niliwauliza kwanini Ukimwi umesambaa sana wakaniambia kuwa ni sababu ya baridi sasa hapa ninyi ni sababu gani?,`` alihoji.
Bila wasiwasi wananchi waliokuwa wakimsikiliza waliitikia kuwa chanzo ni sababu ya supu ya samaki inayopatikana kwa wingi kisiwani humo.
Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwaasa kuacha visingizio kama hivyo na pia waachane na kuendekeza ngono zembe alizosema zinahatarisha maisha yao.
``Wananchi msifanye mzaha na suala hili kwa kuwa tusipofanya jitihada za makusudi kuachana na ngono zembe tutamalizika,`` aliwaasa.
Aidha, alisema serikali inathamini maisha ya wananchi na kila mwaka inatenga fedha nyingi kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kuepukana na janga hilo.
Bw. Lowassa alisema hakuna mwananchi asiyejua madhara ya Ukimwi kwa kuwa karibu kila jamii imeguswa kwa namna moja ama nyingine na madhara haya.
Aliwauliza: ``Hapa nani anaweza kuniambia hajui Ukimwi unaambukizwaje?
Au hajui maana ya Ukimwi.`` Hata hivyo, hakuna aliyejitokeza hali iliyoashiria kuwa wengi wanaufahamu.
Aliwataka viongozi kuendeleza jitihada za kuwakumbusha
__________________
Saturday, October 6, 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment